IQNA

Mjukuu wa Mandela ataka Afrika Kusini ikate uhusiano na Israel

10:56 - August 08, 2017
Habari ID: 3471111
TEHRAN (IQNA)-Mjukuu wa hayati Shujaa Nelson Mandela wa Afrika Kusini ameitaka nchi hiyo ikate uhusiano wote wa kidiplomasia na kibiashara na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Akizungumza Jumapili, Mandla Mandela, ambaye ni mbunge wa chama tawala cha Africa National Congress (ANC), ametoa wito kwa wabunge wa chama hicho kumtimua balozi wa utawala haramu wa Israel nchini humo, Arthur Lenk, na kumuita nyumbani balozi wa Afrika Kuini mjini Tel Avivi, Sisa Ngombane.

"Historia inatuwajibisha tuhuckue hatua sasa na zile zilizochukuliwa na watetezi wa uhuru, uadilifu na amani ambao waliunga mkono harakati ya kimataifa dhidi ya utawala haramu, wa kidhalimu na wa kibaguzi Afrika Kusini,” aliongeza.

Mandla alitoa kauli hiyo baada ya uamuzi wa wabunge kadhaa wa ANC kukataa kukutana na ujumbe kutoka Israel uliokuwa nchini humo.

Mbunge mwandamizi wa ANC Nonceba Mhlauli amesema walipinga ujumbe wa Israel kutembelea Bunge la Afrika Kusini na wakasisitiza kuwa ujumbe huo ukifika bungeni baadaye mwezi huu hawatakutana nao. Chama cha ANC kuna vita 249 katika bunge lenye viti 400.

Jumuiya ya Vyama vya Wafanyakazi Afrika Kusini COSATU nayo pia imeunga mkono hatua ya wabunge hao wa ANC. "COSATU inajiunga na vyama na jumuiya mbali mbali kuunga mkono hatua ya Bunge la Afrika Kusini kukataa kukutana na ujumbe kutoka Israel”

Wazalendo Afrika Kusini wamekuwa wakiunga mkono ukombozi wa Palestina kutokana na kuhsabihiana harakati yao dhidi ya utawala wa makaburi wabaguzi wa rangi na utawala wa kibaguzi wa Israel.

Shujaa Nelson Mandela mwaka 1997 alinukuliwa akisema kuwa, "Uhuru wetu haukamiliki hadi pale Palestina itakapokuwa huru.”

Itakumbukwa kuwa, katika mkutano wa kamati ya sera ya chama cha ANC uliofanyika mjini Johannesburg mwezi JuLAI, chama hicho kilisisitiza kushikamana kwake na taifa la Palestina na kuitaka serikali ipunguze kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ikiwa ni katika fremu ya malengo na misingi ya chama hicho ya kupigani ukombozi.

Hivi karibuni Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusinialisisitiza kuwa, nchi yakeinaunga mkono suala la kuasisiwa nchi huru ya Palestina ili kuhitimisha mzozo wa Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

3463578

captcha