IQNA

Sura Yasin kuwa Maudhui Kuu katika Saa ya Qur’ani Duniani

0:03 - August 15, 2017
Habari ID: 3471123
TEHRAN (IQNA)-Surah Yasin katika Qur’ani Tukufu itakuwa maudhui kuu katika tukio la Saa ya Qur’ani (#QuranHour) ambalo limeandaliwa kimataifa Agosti 31.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ummah Ikhlas Bw. Marhaini Yusoff, amesema harakati hiyo, ambayo katika mitandao ya kijamii inajulikana kama World #QuranHour italipatia kipaumbele Sura Yassin katika Qur’ani Tukufu. Amesema washiriki katika harakati hiyo wanatakuwa kusoma na kuhifadhi Surah Yasin. Aidha amesema washiriki wasiofahamu Kiarabu wanaweza kusoma tarjama za lugha mbali mbali za surah hiyo ya Qur’ani Tukufu.

Aidha ametoa wito kwa washiriki kusambaza video zao wanapoisoma Surah Yasin au kurusha moja kwa moja katika Facebook wakati watakapoisoma katika Saa ya Qur’ani duniani, World #QuranHour.

Saa ya Qur’ani (#QuranHour) ni ubunifu wa mkurungenzi mmoja wa sana nchini Malaysia ambaye anasema lengo lake ni kuwakumbusha walimwengu wote kuhusu mvuto wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

Datuk Rosyam Noor amesema atatumia harakati hiyo, kwa lengo la kuleta umoja katika jamii zote nchini humo.

Amesema kuna fikra potovu kuhusu Uislamu ambapo baadhi wanadhani kuwa Waislamu ni watu wapendao vita na ghasia. ‘Harakati hii inalenga kuondoa fikra mbaya kuhusu Uislamu. Tunataka watu wafahamu kuwa dini haiwezi kunasibishwa na tabia za watu wachache.”

Amesema wasiokuwa Waislamu wanakaribishwa katika harakati hiyo ya ili washuhudie mvuto uliopo katika mafundishi ya Qur’ani Tukufu.

Aidha amesema harakati haiyo ya World #QuranHour itafanyika Agosti 31, kwa minasaba miwili. Awali siku hiyo inatazamiwa kuwa Mahujaji katika Ibada ya Hija watakuwa wakitekeleza amani ya Wukufu huko Arafah na pili Agosti 31 pia ni Siku ya Kitaifa ya Malaysia.

3463626

captcha