IQNA

Hizbullah yalaani ugaidi Uhispania, yasema ISIS inachafua sura ya Uislamu

0:13 - August 19, 2017
Habari ID: 3471129
IQNA (TEHRAN)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, lengo la vitendo vinavyofanywa na kundi la kigaidi la ISIS ni kuchafua haiba na sura halisi ya Uislamu.’

Taarifa hiyo ya Hizbullah imetolewa katika radiamali yake kwa shambulio la kigaidi la Ijumaa katika mji wa Barcelona nchini Uhispania na kusisitiza kwamba, vitendo vya kundi la kigaidi la Daesh havina lengo jingine ghairii ya kuchafua sura ya Uislamu.

Harakati yaHizbullah ya Lebanon sambamba na kulaani shambulio la jana la Daesh katika mji wa Bacelona nchini Uhispania imesisitiza kuwa, jinai hizo ni ishara nyingine ya utendaji wa kigaidi wa kundi hilo.

Aidha Hizbullahimesisitizakwamba, operesheni za kigaidi za kundi la Daesh ni sehemu ya mpango wa kishetani wa kuharibu sura na haiba ya Uislamu.

Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza juu ya udharura wa kupambana na makundi ya kigaidi na kueleza kwamba, hatua ya kwanza ya kuhitimisha jinai za kundi lakigaidi la ISIS ni kuyashinikiza madola makubwa ya Mashariki ya Kati na ya kimataifa ambayo yanaliunga mkono kundi hilola kigaidi.

Katika shambulio la kigaidi la jana huko Barcelona Uhispania dereva wa gari aligonga umati wa watu kwa kukusudia na kuuawatu 13. Watu wenginezaidi ya 100 walijeruhiwa.

Kundi la kigaidi la ISIS limetangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusika na shambulio hilo.

Wakati huo huo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali shambulizi la kikatili na kigaidi lililotokea jana Barcelona huko Uhispania na kusema taifa la Iran linatoa mkono wa pole kwa serikali, taifa na familia za wahanga wa shambulizi hilo.

Bahram Qassemi amesemaq kuwa, ugaidi umekuwa tatizo la ulimwengu mzima na kuongeza kuwa, baada ya kupata kipigo katika medani za vita sasa wamagaidi wa Mashariki ya Kati wamehamishia mashambulizi yao katika maeneo mengine ya dunia na kulenga watu wa kawaida na wasio na hatia yoyote.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, matatizo ya dunia yanahitaji suluhisho la dunia nzima na kuongeza kuwa: Nchi zote zinazopenda amani na wale wenye nia ya kweli ya kupamabana ipasavyo na ugaidi wanapaswa kuunda muungano wa kimataifa wa kukabiliana na ukatili, machafuko na ugaidi na kulipa kipaumbele cha kwanza suala la kung'oa kabisa mzizi wa ugaidi.

3631710

captcha