IQNA

Trump ahimiza Waislamu wauawe kwa risasi zenye damu ya nguruwe

12:01 - August 19, 2017
Habari ID: 3471130
TEHRAN (IQNA)- Rais Donald Trump wa Marekani ametoa matamshi yanayoashiria kutaka Waislamu wauawe kwa kutumia risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe.

Matamshi ya Trump yanakuja kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea mjini Bercelona nchini Uhispania, ambapo watu 13 waliuawa Alhamisi na makumi ya wengine kujeruhiwa. Aidha magaidi watano waliohusika na shambulizi hilo wanaripotiwa kuuawa.

Ijumaa Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa: Jifunzeni mbinu zilizotumiwa na JeneraliPershing wa Marekani baada ya magaidi kukamatwa. Hakukuwa na ugaidiwa Kiislamu kwa muda wa miaka 35", mwisho wa munukuu.

Trump alikuwa akiashiria kisa ambacho wanahistoria wamekitilia shaka kinachoripotiwa kujiri kati ya mwaka(1899–1913) ambapo Jenerali John Pershing wa Marekani aliwakandamizi wafungwa Waislamu wa vuguvugu la uasi laMoro nchini Ufilipinona moja ya mbinu alizotumiani kwa kuwaua wafungwa hao kwa risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe. Waasi hao wa Ufilipinowalikuwa wakipambana naubeberu wa Marekani na uwepo wa majeshi yake nchini mwao.

Hata kabla ya kuingia madarakani, Trump alikuwa anatumia maneno makali yaliyojaa chuki na kejeli dhidi ya Uislamu na Waislamu wakati wa kampeni zake za urais.

Siku chache baada ya kuingia madarakani, bilionea huyo alipasisha agizo la kupiga marufuku kuingia nchini Marekani raia na hata wakimbizi kutoka nchi saba za Kiislamu.

Matamshi ya Trump yanatahtminiwa kuwa ni muendelezo wake wa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3463680

captcha