IQNA

Tamasha La Chakula ‘Halal’ Lafana mjini London

11:59 - August 21, 2017
Habari ID: 3471135
TEHRAN (IQNA)-Tamasha la Chakula Halal limefanyika mjini London kwa mafanikio kati ya Agosti 19-20.
Tamasha La Chakula ‘Halal’ Lafana mjini London

Tamasha hilo, ambalo ni tamasha kubwa zaidi la chakula Halal nchini Uingereza, limewavutia maelfu ya wageni katika siku hizo mbili.

Waliotembelea tamasha hilo walipata maarifa kuhusu vyakula halal na aina mbali mbali ya mapishi. Mashirika mbali mbali yalitumia fursa hiyo kutangaza bidhaa zao halali.

Mbali na Waislamu zaidi ya bilioni 1.5 ambao hutumia chakula Halal duniani, pia kuna watu wengine nusu bilioni wasiokuwa Waislamu ambao hutumia chakula Halal. Hivi sasa biashara ya chakula Halal duniani inakadiriwa kuwa na pato la dola trilioni mbili kwa mwaka. Chakula Halal huwa kinatayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo.

Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Waislamu wanamiliki migahawa, na biashara nyinginezo na pia wanafanya kazi katika sekta za sheria, tiba, teknolojia, usafiri, elimu, vyombo vya habari, sanaa, mitindo n.k.

3463704

captcha