IQNA

11:21 - August 24, 2017
1
News ID: 3471139
TEHRAN (IQNA)-Mamia ya Waislamu wa kabila la Rohingya wamezingirwa na Mabuddha wenye misimamo mikali katika kijiji kimoja kilichoko katika jimbo la Rakhine, magharibi mwa Myanmar.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kwa muda wa wiki kadhaa sasa Waislamu wanaokandamizwa katika kijiji cha Zay Di Pyin wamezuiwa kuondoka katika nyumba zao kutafuta chakula na maji na kufanya kazi.

Taarifa zinasema maafisa wa usalama wa utawala wa Myanmar hawajachukua hatua zozote za maana kuondoa mzingiro huo bali hata wanawahimiza Mabuddha waendelee kuwakandamiza Waislamu hao wanaokadiriwa kuwa 700.

Huku hayo yakiripotiwa, imebainika kuwa maelfu ya Waislamu wa Rohingya wamekimbilia nchi jirani ya Bangladesh baada ya utawala wa Myanmar kuongeza idadi ya wanajeshi katika jimbo la Rakhine. Karibu Waislamu 3,500 wamekimbilia Bangladesh katika wiki za hivi karibuni. Maafisa wa usalama wa Bangladesh wanawazuia wakimbizi hao Waislamu kuingia nchini humo kutokana na kujaa kambi za wakimbizi.

Mwezi Februari mwaka huu Umoja wa Mataifa ulisema mamia ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika ukandamizaji wa miezi ya hivi karibuni katika kile kinachoonekana ni mauaji ya kimbari.

Zeid bin Ra’ad al-Hussein Kamishna wa Haki za Binadamu aktika Umoja wa Mataifa alisema vikosi vya usalama Myanmar vimetekeleza mauaji ya umati, ubakaji wa Waislamu kigenge na kuteketezwa vijiji vyao katika kampeni mpya ya ukandamizaji iliyoanza mwezi Okotba mwaka jana.

Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wamerekodi vitendo vipya ya ukatili ikiwa ni pamoja na mateso, utekaji nyara, ubakakji wa kigenge na mmauaji ya watoto wachanga, kwa mfano miezi minane, mikononi mwa jeshi la Myanmar.

Mapema mwezi huu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka serikali ya Myanmar kuheshimu haki za Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3463727

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
swaleh said
0
0
Kwanini mayaifa ya kiislamu hayaungani kuwapa hifadhi na kuwasaidia bali kuzozana wao kwa wao? Tukumbuke tuna mas ulia mbele ya mwenyezi mungu kesho akhera kutowasaidia. Allah yaa'lam.
Name:
Email:
* Comment: