IQNA

Wasiwasi wa Mahujaji kuhusu sera za kupinga Uislamu za rais Trump wa Marekani

11:26 - September 03, 2017
Habari ID: 3471154
TEHRAN (IQNA)-Mahujaji kutoka Marekani, Uingereza na Canada walioshiriki katika Ibada ya Hija wamebainisha wasiwasi wao kuhusu sera za chuki dhidi ya Waislamu za Rais Donald Trump wa Marekani.

Katika mahojiano na kanali ya Al Jazeera mjini Makka wengi wamesema wanaishi maisha yaliyojaa wasiwasi pasina kujua ni kipi kitakachopjiri.

"Watu wamekasirika, wana huzuni na wasiwasi," amesema Yasir Qadhi, msomi wa Kiislamu ambaye amesafiri kutoka jimbo la Tennessee kwa ajili ya Ibada ya Hija.

Akiwa mgombea kiti cha urais, Trump alipendekeza Waislamu wapigwe marufuku kuingia Marekani. Alipochukua hatamu za uongozi Januari mwaka huu aliwapiga marufuku wasafiri kutoka nchi zenye Waislamu wengi kuinia Marekani. Hatahivyo amri hiyo imepingwa na mahakama ambazo zinasema ni ya kibaguzi.

Mmarekani Wajahat Ali aliyepata taufiki ya kutekeelza Ibada ya Hija anasema yeye na wenzake wamemuomba Mwenyezi Mungu awasahilishie Waislamu wa Marekani katika kipindi hiki kigumu huku akiwa na matumaini kuwa hali itaboreka.

3463821

captcha