IQNA

12:53 - September 04, 2017
News ID: 3471157
TEHRAN (IQNA)-Utawala wa Mabuddha wenye misimamo mikali nchini Myanmar umewaua kwa umatu Waislamu karibu 3,000 huku taasisi zote za Umoja wa Mataifa za kuwafikishia misaada ya dharura Waislamu zikizuiwa.

Taarifa zinasema kipindi cha kuanzia Agosti 25 hadi 27 jeshi la Myanmar liliwaangamiza kwa umati Waislamu zaidi ya 3,000. Hayo ni kwa mujibu wa Anita Schug Baraza la Rohingya Barani Ulaya, ambayo anasema Waislamu kati ya 2,000 and 3,000 waliuawa katika kipndi cha siku tatu nchini Myanmar. "Hali katika jimbo la Rakhine inaashiria mauaji ya kimbari yanayojiri hatua kwa hatua," amesema Schug huku akilituhumu Jeshi la Myanmar kwa kuhusika na mauaji ya Waislamu. Wakimbizi Waislamu kutoka Myanmar waliopata hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh wanasimulia kile wanachokitaja kuwa ni mauaji ya kuogofya yanayotekelezwa na jeshi na Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu ada.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na yametangaza kusitisha ufikishaji misaada ya chakula, dawa na maji kwa Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaokandamizwa katika jimbo la Rakhine kufuatia mapigano mapya yaliyoibuka Agosti 25.Hiyo ni baad aya serikali ya Myanmar kuzuia mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa

Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile UNHCR, UNFP, UNICEF na WFP wamezuiwa na utawala wa Myanmar kufanya kazi katika jimbo lenye Waislamu wengi la Rakhine na hivyo kupelekea watu zaidi ya robo milioni kukosa chakula na dawa.

Pamoja na kuwepo ushahidi wa mauaji ya kimbari ya Waislamu na hata baada ya kuzuiwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kuingia katika jimbo la Waislamu la Rakhine nchini Myanmar, jamii ya kimataifa haijachukua hatua zozote za maana na imefumbia macho ukandamizaji huo wa Waislamu. Halikadhalika vyombo vya habari vya Magharibi pia kwa ujumla vimepuuza mauaji ya Waislamu nchini Myanmar huku baadhi wakidai kuwa eti waliouawa ni magaidi.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za jirani kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3638142

Tags: iqna ، Waislamu ، Myanmar ، mauaji ، Rakhine
Name:
Email:
* Comment: