IQNA

Rais Hassan Rouhani wa Iran
16:33 - September 20, 2017
News ID: 3471184
TEHRAN (IQNA)-Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hali ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar ni ya kusikitisha huku akisisitiza udharura wa kuishinikiza serikali ya Myanmar ili isitishe mauaji ya kimbari na ukandamizaji dhidi ya Waislamu Warohingya.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran ametoa wito huo katika kikao cha Kundi la Mawasiliano la OIC kilichofanyika mjini New York na kusisitiza kwamba serikali ya Myanmar inapaswa ijue kuwa kuwafukuza watu katika nchi yao na kuwafanya wakimbizi katika nchi nyinginezo sio suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo.

Dakta Rouhani ameeleza kwamba serikali ya Myanmar inatakiwa iponye machungu ya muda mrefu ya jamii ya Waislamu wa nchi hiyo kwa kuchukua hatua athirifu za kuwarejeshea haki zao za kiraia.

Mbali na kusisitiza kuwa Iran iko tayari wakati wowote kutoa msaada kwa Waislamu madhulumu wa Myamnar, Rais Rouhani amebainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono njia yoyote ya ufumbuzi itakayodhamini kuheshimiwa kikamilifu haki za binadamu, hadhi ya utu na usalama wa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar.

Wakati huo huo,Rais  Rouhani amesema hali ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar ni ya kusikitisha huku akisisitiza udharura wa kuishinikiza serikali ya Myanmar ili isitishe mauaji ya kimbari na ukandamizaji dhidi ya Waislamu Warohingya.

Rais Rouhani aliyasema hayo mjini New York wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Stefan Löfven Waziri Mkuu wa Sweden pembizoni mwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Ameongeza kuwa, Waislamu wa Myanmar wanakabiliwa na hali ngumu na kuongeza kuwa: "Umoja wa Ulaya unaweza kuwa na nafasi muhimu katika kusitisha ukandamizaji wa Waislamu wa Myanmar na kuwasaidia wakimbizi katika jamii hiyo."

3463959Name:
Email:
* Comment: