IQNA

Waislamu Tanzania katika maombolezo ya Imam Hussein AS+PICHA

10:18 - September 26, 2017
Habari ID: 3471192
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wanajumuika katika Msikiti wa Al Ghadir mjini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya maombolezo ya kuuawa Imam Hussein AS katika mwezi wa Muharram.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu wa matabka mbali mbali, aghalabu wakiwa Waislamu wa madhehebu ya Shia wanashriki katika majlisi hizo za maombolezo ya Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS. Kati ya wageni wa heshima wanaoshiriki katika mambolezo hayo ambayo yanafanyika katika siku 10 za kwanza za Mwezi wa Muharram ni Balozi wa Iran nchini Tanzania Mheshimiwa Musa Farhang na mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Bagheri na pia Mkuu wa Chuo Kiuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW tawi la Tanzania.

Hotuba katika majlisi hizo za maombolezo zinatolewa na Maulana Sheikh Hemed Jalala Imam wa Masjid Al Ghadir na kiongozi wa Chuo cha Dini ya Kiislamu cha Imam Swadiq AS mjini Dar es Salaam.

Itakumbukwekuwa miaka 1378 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura ambayo ni siku ya 10 ya Mwezi wa Muharram. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili la Yazid bin Muawiya ili kuilinda dini ya Allah SWT.

Waislamu Tanzania katika maombolezo ya Imam Hussein AS


Waislamu Tanzania katika maombolezo ya Imam Hussein AS


Waislamu Tanzania katika maombolezo ya Imam Hussein AS


Waislamu Tanzania katika maombolezo ya Imam Hussein AS


3646495

captcha