IQNA

10:47 - September 26, 2017
News ID: 3471193
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu Misri Sheikh Mohamed Mokhtar Gomaa amesema wizara yake itaanzisha shule za Qur’ani katika misikiti yote mikubwa nchini humo.
Shule za Qur’ani kuanzishwa katika misikiti yote mikubwa MisriSheikh Gomaa amebaini kuwa, moja ya shule hizo itazinduliwa hivi karibuni katika Msikiti Mkuu wa Cairo katika kipindi cha siku chache zijazo. Ameongeza kuwa, wizara yake itagharamia ujenzi wa shule hizo katika misikiti na kwamba Maimamu wa misikiti na walimu wa Qur’ani ndio watakaosimamia shule hizo.

Sheikh Gomaa amebainisha kuwa wanafunzi katika shule hizo hawatatozwa karo na kwamba wanaofunza katika shule hizo wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na wasiwe na misimamo mikali ya kidini.

Misri ni nchi iliyo kaskazini mwa Afrika na ina idadi ya watu karibu milioni 95 ambapo Waislamu ni asilimia 90 ya watu wote nchini humo. Harakati Za Qur’ani nchini Misri zina historia ndefu inayonawiri na nchi hiyo inaongoza kwa quraa au wasomaji bora wa Qur’ani duniani.

3646073

Name:
Email:
* Comment: