IQNA

13:14 - September 27, 2017
1
News ID: 3471195
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amekwenda katika Msikiti wa Imam Husain AS hapa Tehran na kuusomea Faatiha mwili mtoharifu wa shahid Mohsen Hojaji, aliyeuliwa shahidi na magaidi wa Daesh au ISIS wakati akilinda Haram ya mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW, Bibi Zaynab al Kubra AS nchini Syria.

Kwa mujibu wa taarifa, katika mahojiano aliyofanyiwa baada ya kumsomea Faatiha shahid huyo, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemsifu shahid Hojaji kwa kujitolea kwake katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumuomba Allah ampandishe daraja za juu za utukufu kama ambavyo pia amemuomba Mwenyezi Mungu azidishe subira na uvumilivu katika nyoyo za watu wa familia yake.

Shughuli ya kumuaga shahid Mohsen Hojaji imefanyika leo hapa Tehran na baadaye mwili wake utapelekwa kijijini kwao katika mkoa wa Isfahan wa katikati mwa Iran kwa ajili ya maziko hiyo kesho Alkhamisi.

Tarehe 9 Agosti 2017, kundi la kigaidi la ISIS lilimuua shahidi kijana huyo muumini ambaye kwa mapenzi yake makubwa kwa watu wa nyumba tukufu ya Bwana Mtume Muhammad SAW alikwenda nchini Syria kulinda haram za watukufu hao zisinajisiwe na magenge ya kigaidi kama vile Daesh au ISIS.

3647030

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
MOHAMED RUCKER ABDULRAMAN
0
0
asalam aleikum.Niko kenya sehemu ya pwani mtwapa habari
zenu na zipenda zina zindua mambo mengi juu ya uislam unavyo pigwa vita dhidi ya uzayuni.Tuko pamoja
Name:
Email:
* Comment: