IQNA

13:27 - September 28, 2017
1
News ID: 3471197
TEHRAN (IQNA)-Polisi katika mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China wameamuru familia za Waislamu kukabidhi madhihirisho ya kidini hasa nakala za Qur'ani na misala.

Taarifa zinasema maafisa wa usalama katika mkoa Xinjiang, ambao wakazi wake waliowengi ni Waislamu, wamekuwa wakizinguka katika mitaa na misikiti huku wakiwatisha Waislamu. Walioshuhudia wanasema Waislamu wa makabila au jamii za Uyghur, Kazakh na Kyrgyz wametakiwa kuwakabidhi maafisa wa usalama nakala za Qur'ani na misala wanayomikili majumbani mwao na watakaokiuka amri hiyo watachukuliwa hatua.

"Maafisa wa kijiji, mji mdogo na kaunti wanawapokonya Waislamu nakala zote za Qur'ani na misala," amesema Muislamu wa jamii ya Kazakh katika eneo la Altay ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa hofu ya kukamatwa. Akizungumza Jumatano na kusema karibu kila nyumba ya Muislamu katika eneo hilo ina nakala ya Qur'ani na pia mkeka au msala.

Kwa mujibu wa Dilxat Raxit, msemaji wa Jumuiya ya Kimataifa ya Jamii ya Uygur, amri hiyo ya kuwakadamiza Waislamu imeanza kutekelezwa mapema mwezi huu wa Septemba.

"Tumepokea taarifa kuwa watu wote wa jamii wa Uyghur wametakiwa kukabidhi maafisa wa polisi kila kitu kinachohusiana na Uislamu ikiwa ni pamoja na nakala za Qur'ani, mikeka ya kusalia na nembo yoyote ile ya Kiislamu," alisema Raxit. Amesema Waislamu wengi wamelazimika kukabidhi nakala zao za Qur'ani na misala kwa kuhofia kuchukuliwa hatua kali.

Hii si mara ya kwanza kwa wakuu wa mkoa wa Xinjiang nchini China kuwakandamiza Waislamu. Mwaka jana watawala wa eneo hilo waliwaamuru wanafunzi, wafanya kazi wa umma na hata wakaazi wa kawaida kutofunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Aidha Waislamu wa eneo hilo walipigwa marufuku kuwapa watoto wao baadhi ya majina ya Kiislamu

Chama tawala cha Kikomunisti cha China kwa miaka kadhaa sasa kimekuwa kikiwakandamiza Waislamu katika eneo la Xinjiang.

3647555

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
mvano
0
0
Hiyo ndio mitihani ya waislam ili Allah anawapima waliowaumini wa kweli kama alivyowapima waliokuwepo kabla yetu. Allah amesajili aina ya mitihani hiyo katika Qur an.
Ni jukumu letu kuwaombea Allah awanusuru.
Name:
Email:
* Comment: