IQNA

20:17 - September 30, 2017
News ID: 3471199
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani wanashiriki katika maadhimisho ya Siku ya Tasu'a, wakifanya maombelezo ya kukumbuka mapambano ya Karbala yaliyopelekea kuuawa shahidi Imam Hussein AS.

Huku aghalabu wakiwa wamevalia mavazi meusi kama ishara ya maombolezo, Waislamu hasa wa Madhebu ya Shia katika kona zote za dunia wanahudhuria kwa wingi kwenye Husainia, Misikiti, mitaani na majumbani kwa ajili ya maadhimisho ya Tasu'a, siku moja kabla ya Siku ya Ashuraa kuuawa shahidi Imam wa 3 Hussein AS na wafuasi wake na askari katili wa utawala dhalimu wa Bani Umayya, mwaka 680 Hijria. Kilele cha maadhimisho hayo kimekuwa nchini Iraq ambapo mamilioni ya watu kadhalika wamekusanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala kushiriki kumbukizi hiyo ya tukio chungu la kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW.

Siku ya Tasu'a ambayo pia inafahamika kama 'Siku ya Mapambano' ni siku ya kumuenzi Abbas Ibn Ali, ndugu wa Imam Hussein AS kutokana na namna alivyojitolea kufa kupona katika mapambano ya Karbala.

Tarehe 10 Muharram yaani kesho Jumapili, ni siku ya Ashura, siku ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu huyo wa Bwana Mtume Muhammad SAW akiwa pamoja na wafuasi wake wapatao 72, katika jangwa la Karbala, karibu karne 14 zilizopita.

3464038

Tags: iqna ، shirika la habari la qurani ، shia ، ، ، ، ، ،
Name:
Email:
* Comment: