IQNA

14:50 - October 03, 2017
News ID: 3471202
TEHRAN (IQNA)- Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) limechukua uamzui wa kihistoria wa kuondoa marufuku ya muda mrefu ya wanawake Waislamu kuvaa Hijabu wanapocheza.
FIBA yaondoa rasmi marufuku ya Hijabu katika mpira wa kikapu dunianiUamuzi huo ambao ulichukuliwa mwezi Mei na shirikishilo hilo la mchezo wa mpira wa kikapu (basketboli) duniani umeanza kutekelezwa rasmi Jumapili wiki hii baada ya kampeni ya muda mrefu katika mitandao ya kijamii. FIBA pia imeondoa marufuku ya vilemba na kofia za kidini kwa wachezaji wa kulipwa.

Tokea mwaka 2015 FIBA imekuwa ikiruhusu kwa majaribio wanawake Waislamu wacheze basketiboli wakiwa wamevaa Hijabu. Mwezi Mei mwaka huu FIBA ilitangaza kuwa itairuhusu timu ya basketboli ya wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kucheza wakiwa wamevaa Hijabu.

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Basketboli ya Iran kwa muda mrefu haikuwa ikishiriki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu kutokana na FIBA kupiga marufuku wanawake wanaovaa Hijabu kushiriki katika mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

Nchini Uingereza timu ya wanawake Waislamu ya basketboli ijulikanayo kama Falcons ya mjini Leicester Uingereza imefurahiswha na uamuzi huo. "Uamuzi wa FIBA ni muhimu kwani wote wataweza kuona kuwa wanawake Waisalmu wanaweza kucheza, wanacheza na wana irada ya kucheza," amesema Raabya Pasha, mwanachama wa timu hiyo. "Hata tukijistiri, hilo halituzuii kucheza," ameongeza. Naye Asma Elbadawi, kocha na msimamizi wa timu ya Falcons, na ambaye aliongoza kampeni ya mitandao ya kijamii ya kutoka FIBA iondoe marufuku ya Hijabu, anasema ana matumaini kuhusu mustakabali. "Pengine hasa hatuwezi kuhisi mabadiliko, lakini katika siku za usoni tutawaona wasichana wengi wakicheza basketboli wakiwa wamevaa Hijabu hata nchini Marekani."

3464060

Name:
Email:
* Comment: