IQNA

Magaidi wa ISIS watimuliwa kutoka ngome yao ya mwisho Iraq

23:08 - October 06, 2017
Habari ID: 3471206
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Iraq limefanikiwa kuukomboa mji wa kistratijia wa Hawija ambao ulikuwa ngome kuu ya mwisho ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Jeshi la Iraq lilisema mji wa Hawija ulio katika mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Kirkuk kaskazini mwa nchi hiyo, umekombolewa baada ya wiki kadhaa za mapigano makali na magaidi wa ISIS waliokuwa wameteka mji huo.

Aidha imedokezwa kuwa, kufuatia kukombolewa Hawija, hivi sasa eneo pekee ambalo limebakia mikononi mwa ISIS ni kipande kidogo cha mpaka wa magharibi mwa Iraq na Syria. Awamu ya kwanza ya kuukomboa mji wa Hawija, ulio umbali wa kilomita 300 kutoka Baghdad, ilianza Septemba 21. Mnamo Septemba 29 Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi alitangaza kuanza awamu ya pili ya oparesheni ya kuukomboa mji huo.

3464085

captcha