Ongezeko la watalii Waislamu katika miaka ya hivi karibuni nchini Japan limeambanatana na kuongezeka idadi ya migahwa yenye kuuza chakula halali. Hivi sasa katika viwanja vya ndege na hoteli kubwa nchini Japan kuna migahawa yenye vyakula halali. Migahawa hiyo mbali na kupika chakula halali inapika vyakula maalumu kutoka nchi za Waislamu kama vile Bangladesh, Misri, Indonesia, Iran, Malaysia, Morocco, Pakistan na Uturuki.
Aidha Waislamu wanaOishi Japan wanaweza kununua nyama halali iliyochinjwa kutoka nchi za kusini wa Asia kama vile Indonesia au Malaysia. Kutokana na kuwa Uislamu ni dini ya pili kwa wingi wa wafuasi duniani sambamba na kuwa dini inayenea kwa kasi zaidi duniani, soko la bidhaa na huduma halali litaendelea kupanuka. Soko la bidhaa za Kiislamu lilikuwa na thamani ya dola trilioni 2.6 mwaka 2015 na linatarajiwa kuimarika zaidi huku Waislamu wengi wakiwa wanasisitiza kufuata mafundisho ya Kiislamu katika maisha yao ya kila siku. Kwa msingi huo, nembo ya ‘Halal’ itakuwa sehemu ya biashara nyingi hasa za vyakula, hoteli, benki, bima na masoko ya hisa.
3464226