Abdullah al-Jurjawi ametajwa kuwa mtu mwenye umri wa juu zaidi kufanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu mjini Jeddah katika mwaka 1438 Hijria Qamaria (2016/2017).
Katika mahojiano na gazeti la Okaz la Saudia, amesema tokea zama za ujana wake alikuwa anasoma kurasa mbili za Qur'ani kila siku lakini alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu baada ya kustaafu mwaka jana.
"Punde baada ya kustaafu, nilimfuata Ustadh Majid Bijash katika Msikiti wa Ahl al-Khair, na Alhamdulillah, nilifanikiwa kuhifadhi Qur'ani kwa muda wa miezi 10."
Tayari al-Jurjawi ameshafanya mtihani wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Jumuiya ya Qur'ani ya Khayrukum mjini Jeddah.
Jumuiya hiyo imesema itamuenzi kikamilifu al-Jurjawi katika hafla maalumu siku za usoni.