IQNA

Bangladesh yaitaka dunia iishinikize Myanmar iache kuwakandamiza Waislamu

18:19 - November 05, 2017
Habari ID: 3471248
TEHRAN (IQNA)-Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuishinikiza Myanmar isitishe ukandamizaji wa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.

Aidha ameitaka jamii ya kimataifa isaidie kuwarejesha nyumbani wakimbizi zaidi ya laki sita Warohingya waliokimbilia Bangladesh kufuatia ukandamizaji nchini Myanmar.

Sheikh Hasina ameyasema hayo Jumapili katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka wakati akifungua mkutano wa 63 wa kibunge wan chi za Jumuiya ya Mdola na kuongeza kuwa, kukandamizwa Warohingya kumevuruga uthabiti katika eneo hilo.

Hasina ameashiria hali mbaya ya wakimbizi 622,000 Warohingya kutoka Myanmar waliongia nchini Bangladesh tokea Agosti 25 na wengine zaidi ya 400,000 ambao waliingia nchini humo nyakati tafauti tokea mwaka 1978.

Waislamu wa Rohingya wa Myanmar zaidi ya elfu sita wameshauawa na wengine zaidi ya elfu 10 kujeruhiwa hadi sasa tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu wakati lilipoanza wimbi jipya la mashambulizi ya ukandamizaji ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya jamii hiyo ya walio wachache katika mkoa wa Rakhine.

3464340

captcha