IQNA

‘Siku ya Kuvaa Hijabu’ katika Chuo Kikuu cha Marywood, Marekani

11:23 - November 07, 2017
Habari ID: 3471253
TEHRAN (IQNA)-Chuo Kikuu cha Marywood katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani kimepanga kuandaa ‘Siku ya Kuvaa Hijabu’ mnamo Novemba 15.

"Lengo la siku hii ni kuonyesha umoja, na kuwaunga mkono wasichana wanaovaa Hijabu; kuvaa Hijabu hakumaanishi kusilimu. Kuvaa Hijabu katika siku hiyo ni kuonyesha mfungamano,” amesema Salma Ahmed, mwanachuo wa taaluma ya lishe ambaye ni kati ya wanaoandaa Siku ya Hijabu chuoni hapo.

Kabla ya Siku ya Hijabu chuoni hapo kutafanyika kikao cha kubainisha kuhusu umuhuimu wa Hijabu katika Uislamu na pia kuwafunza wasiokuwa Waislamu namna ya kuvaa Hijabu.

Salma Ahmed anasema aliamua kuandaa Siku ya Kuvaa Hijabu baada ya wananfunzi wengi kumtaka awafahamishe umuhimu wa vazi hilo huku wengi wakiwa na hamu ya kuvaa vazi hilo stara.

Kufuatia wimbi la chuki dhidi la ya Uislamu katika nchi za Magharibi Waislamu sasa wanatumia mbinu mbali mbali za kuelimisha jamii kuhusu Uislamu ili kuondoa dhana potofu zilizopo na wamefanikiwa kuwaongoza wengi katika njia ya haki au kubadilisha mitazamo yao hasi.

3464348

captcha