IQNA

Magenge ya wenye chuki dhidi ya Uislamu Ulaya wapata mafunzo ya kijeshi

13:13 - November 08, 2017
Habari ID: 3471254
TEHRAN (IQNA)-Vijana Wazungu Waingereza wenye misimamo ya kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu wanapata mafunzi ya kijeshi, televisheni ya ITV imefichua.
Magenge ya wenye chuki dhidi ya Uislamu Ulaya wapata mafunzo ya kijeshiKatika kuchunguza kadhia hiyo, Televisheni ya ITV iliwatuma wanawake watatu kikachero ambao walijiunga na makundi ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali likiwemo kundi linalopinga wahamiaji la Generation Identity.

Kundi hilo linalenga kuleta pamoja harakati za kitaifa za vijana Wazungu Ulaya ili kulina kile wanachosema ni kuhatarishwa utambulisho na utamaduni wa Wazungu barani Ulaya kufuatia ongezeko la wahamiaji na kuenea Uislamu barani huo.

ITV imeerusha hewani filamu inayowaonyesha vijana hao wenye misimamo mikali wakiwa Ufaransa kupata mafundisho yanayoshabihiana na ya kijeshi katika kambi za kundi la Generation Identity.

Kuongezeka wimbi la vyombo vya habari vinavyoeneza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya kumewaweka katika wakati mgumu sana Waislamu barani humo kiasi kwamba uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa, kati ya kila watu watano wa barani Ulaya, mmoja anachukia kuwa na jirani Muislamu.

3464367

captcha