IQNA

Mamilioni katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS, Karbala, Iraq

9:42 - November 09, 2017
Habari ID: 3471255
TEHRAN, (IQNA)-Leo mamilioni ya watu wanashiriki katika maombolezo kwa munasaba wa Arubaini ya Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS, ambapo kilele cha maombolezo hayo ni Karbala, Iraq.

Mamillioni ya wafanyaziara kutoka maeneo yote duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wamefika katika mji wa Karbala, Iraq kwa ajili ya kushiriki katika maombolezo ya siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Hapa nchini Iran pia mamilioni ya wananchi wanashiriki katika hafla mbali mbali za maombolezo ya Arubainizilizoandaliwa katika misikiti, kumbi za kidini maarufu kama Husseiniya na pia katika mitaa mbali mbali

Inafaa kukumbusha kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifuya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Mwaka huu wa 1439 Hijria Qamaria, Arubaini itakuwa tarehe 20 Safar sawa na Novemba 9, 2017 ambapo mamilioni ya wafanya ziara kutoka maeneo yote ya dunia wamefika Karbala kwa ajili ya ziara hiyo ya Arubaini.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) linatoa salamu za rambi rambi kwa Waisalmu wote hasa Mashia duniani, na wapenda uhuru kwa munasaba huu wa kuwadia Arubaini ya Imam Hussein AS.



Mamilioni katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS


Mamilioni katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS



Mamilioni katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS

3466657

captcha