IQNA

Waislamu wakasirishwa na matamshi ya waziri Bahrain kuhusu Quds Tukufu

11:43 - December 22, 2017
Habari ID: 3471320
TEHRAN (IQNA)-Waislamu maeneo mbali mbali duniani wamebaiisha hasira zao kufuatia matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain aliyeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa eti kadhia ya Quds na Palestina si muhimu bali ni suala la pembeni tu.

Waislamu katika mitandao mbali mbali ya kijamii wamelaani vikali kiongozi huyo wa ngazi za juu kwa sababu ya upuuzaji aliodhihirisha kuhusu Quds Tukufu (Jerusalem), kibla cha kwanza cha Waislamu.

Akijibu hatua hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Aal Khalifa, Bahram, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi amesema, licha ya kuweko njama na hila za kila namna za kuzusha migogoro bandia, lakini kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala muhimu zaidi kwa ulimwengu wa Kiislamu hadi zitakapokombolewa ardhi zote za taifa hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain amedai katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hakuna haja ya kujiingiza katika mgogoro na Marekani katika suala la Palestina. Itakumbukwa kuwa ukoo wa Aal Khalifa sawa na Aal Saud ni vibaraka wakuu wa Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, hakuna mtu wala nchi yoyote inayoweza kuitoa kadhia ya Palestina katika moyo wa umma wa Kiislamu kwani Palestina ni sehemu muhimu sana ya ulimwengu wa Kiislamu.

Suala la Palestina si muhimu tu kwa ulimwengu wa Kiislamu, bali ni kadhia muhimu kwa dunia nzima. Jana Alkhamisi, wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipasisha kwa kura mutlaki muswada wa kuiunga mkono Quds na kudharau vitisho vyote vilivyotolewa na Marekani kura hiyo.

3674963

captcha