IQNA

Washiriki 70 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Sudan

23:05 - December 29, 2017
Habari ID: 3471330
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sudan yanatazamiwa kufanyika wiki ijayo na yatakuwa na washiriki 70.

Kwa mujibu wa Maaz Fatih al-Hajj, mmoja kati ya wasimamizi wa mashindano hayo, washiriki hao 70 watashindana katika vitengo viwili tafauti vya wanawake na wanaume.

Ameongeza kuwa, pembizoni mwa mashindano hayo kutakuwa na semina kadhaa pamoja na hafla za kiutamaduni. Aidha kutakuwa na mihadhara kuhusu miujiza ya Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW na kati ya watakaohutubu ni mwanazuoni mashuhuri wa Misri Sheikh Omar Abdul Kafi Shihatta.

Mashindano ya Tisa ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sudan, maarufu kama Zawadi ya Khartoum, yataanza Januari 5-12 mwaka 2018.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemteua Mohammd Rasoul Takbiri kuwa mwakilishi wake katika mashindano hayo.

Mwaka uliopita mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani yalikwua na washiriki 74 kutoka nchi 55.

 

3676870

 

captcha