IQNA

Nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu zasambazwa Djibouti

10:38 - January 08, 2018
Habari ID: 3471346
TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu imezawadia watu wa Djibouti nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maafisa wa jumuiya hiyo wamekabidhi nakala hizo za Qur’ani Tukufu kwa maafisa wa wizara ya elimu ya Djibouti katika sherehe zilizofanyika mjini Djibouti.

Wakuu wa wizara hiyo wameishukuru Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu kwa kutoa zawadi ya nakala hizo za Qur’ani huku wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha elimu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Inatazamiwa kuwa nakala hizo za Qur’ani zitasambazwa miongoni mwa wanafunzi katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu amesema kuna mpango wa kuanzisha ‘Kituo cha Elimu na Ustawi’ Djibouti kupitia ufadhili wa jumuiya yake kwa lengo la kuboresha elimu katika nchi hiyo ndogo ya Kiislamu. Amesema kituo hicho kutakuwa kinatoa kozi kadhaa za teknolojia na fani nyinginezo zinazohitajiwa na vijana wa nchi hiyo.

Djibouti ni nchi ndogo ya iliyo katika Pembe ya Afrika na ina idadi ya watu takribani milioni moja ambapo zaidi ya asilimia 95 ni Waislamu. Lugha rasmi nchini humo ni Kiarabu na Kifaransa huku lugha za kitaifa zikiwa ni Kisomali na Kiafar.

3678899/

captcha