IQNA

Hafidh wa Qur'ani wa Morocco ashinda mashindano ya Qur'ani Sudan

11:12 - January 15, 2018
Habari ID: 3471355
TEHRAN (IQNA)-Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Morocco ametangazwa mshindi katika Mashindano ya Tisa ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Sudan na kutunukiwa zawadi yake Jumamosi usiku.

Jopo la majaji walimtangaza Ahmed Abdul-Wahhab Ashiri kutoka Morocco kuwa mshindi wa mashindano hayo ambayo pia ni maarufu kama Zawadi ya Khartoum.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Muhammad Ahmed wa Sudan huku Salim Abdullah Alim wa Libya akichukua nafasi ya tatu. Zawadi za washindi watatu wa kwanza zilikuwa ni dola $40,000, $30,000 na $25,000 kwa taratibu.

Wawakilishi wa Nigeria, Kenya, Mauritania, Syria, Iran, Sudan na Bangladesh walichukua nafasi za nne hadi 10 kwa taratibu.

Jumla ya washiriki 73 waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 50 ambao walifika mjini Khartoum kushiriki katika mashindano hayo yaliyoendelea kwa muda wa wiki moja.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliwakilishwa katika mashindano hayo na Hafidh Mohammad Rasul Takbiri.

Pembizoni mwa mashindano kulikuwa na semina kadhaa pamoja na hafla za kiutamaduni. Aidha kulikuwa na mihadhara kuhusu miujiza ya Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW.

3681683

captcha