IQNA

Muhula wa kutuma Makala katika Kongamano la Kimataifa la Qur'ani waongezwa

14:53 - January 20, 2018
Habari ID: 3471363
TEHRAN (IQNA)-Muhula wa kuwasilisha makala katika Kongamano la 11 la Kimataifa la Masomo ya Qur'ani Iran umeongezwa hadi Machi 11.

Kwa mujibu wa waandalizi wa kongamano hilo, wale wanaotaka kutuma makala kwa lengo la kushiriki katika kongamano wanaweza kuzituma kupitia tovuti ya intaneti ya www.iqro.ir au kupitia barua pepe ya quranicconference@gmail.com.

Awali Februari 19 2018 ilikuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha makala kwa wanaotaka kushiriki katika kongamano hilo litakalofanyika mwezi Aprili.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafundisho ya Qur'ani kilichoko mjini Qum, Iran huandaa kongamano hilo kila mwaka katika kipindi cha kufanyika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Chuo hicho kikuu kinafungamana na Shirika la Wakfu la Iran ambalo huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Maudhui kuu ya Kongamano la 11 la Kimataifa la Masomo ya Qur'ani  mwaka huu ni 'Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa."

Washiriki watajadili mapambano dhidi ya uistikbari kwa matazamo wa Qur'ani Tukufu na Ahul Bayt AS na pia katika sera za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

3683398

captcha