IQNA

Ukandamizaji Bahrain walaaniwa na mashirika ya haki za binadamu, UN, Magharibi kimya

21:20 - February 03, 2018
Habari ID: 3471379
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain unaendelea kutekeleza sera za ukandamizaji dhidi ya wapinzani ikiwa ni pamoja na kuwanyonga, kuwatesa, kuwapokonya uraia na kuwalazimui kuihama nchi huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakinaani uovu huo ambao umenyamaziwa kimya na Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi.

Ukandamizaji Bahrain walaaniwa na mashirika ya haki za binadamu, UN, Magharibi kimyaSiku chache zijazo, utamalizika mwaka wa saba tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kiimla nchini humo. Itakumbukwa kuwa Februari mwaka 2011, wananchi wanamapinduzi wa Bahrain walianzisha mwamko mkubwa wa Kiislamu dhidi ya utawala wa ukoo wa Aal Khalifa na tokea wakati huo maadanmano ya amani yamekuwa yakiendelea takribani kila siku huku utawala ukitumia mkono wa chuma kuwakandamiza wananchi.

Ukatili waongozeka

Nukta muhimu hapa ni kuwa, kudumu kwa muda mrefu mgogoro wa Bahrain si tu kuwa hakujapelekea utawala wa Aal Khalifa kutafuta njia muafaka ya kisiasa ili kuzia kuendelea maandamano yanayojumuisha zaidi ya nusu ya watu wote nchini humo, bali kadiri muda unavyosonga utawala huo unazidi kuonyesha mabavu na ukatili zaidi dhidi ya wananchi. Sababu kuu ya kiburi cha utawala wa Aal Khalifa ni kuwa, kijiografia, Bahrain ina umuhimu mkubwa kwa Saudi Arabia, Marekani na Uingereza. Maslahi ya tawala hizo tatu yanaweza kudhaminiwa tu kwa kuendelea kubakia madarakani utawala wa kiimla uliopo Bahrain. Kwa msingi huo si tu kuwa jamii ya kimataifa haichukui hatua yoyote kujaribu kusitisha jinai za utawala wa Aal Khalifa bali kimya mbele ya jinai hizo ni sawa na kuidhinisha kuendelea ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za baindamu katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Madola ya magharibi yanaunga mkono ukatili Bahrain

Kutokana na uungaji mkono huo wa madola ya Magharibi ambayo yana vituo vya kijeshi Bahrain, utawala wa Aal Khalifa unazidi kupanua wigo wa ukandamizaji na jinai dhidi ya wananchi wanaoandamana kwa amani. Ni kwa msingi huu ndio tarehe 28 na 29 Januari, utawala wa Aal Khalifa uliwalazimu ndugu wanne Wabahraini wahame nchi na kuelekea Iraq. Kwa hivyo kile kinachojiri hapa ni kuwalazimu Wabahrain wahame nchi yao na kwa msingi huo kuwapokonya uraia. Utawala wa Aal Khalifa unawapokonya Wabahrain uraia katika fremu ya 'maangamizi ya kimbari' nchini humo. Wanaolengwa katika maangamizi hayo ya kimbari ni Wabahrain waliowengi ambao ni Waislamu wa madhehebu ya Shia. Utawala wa kiimla wa Bahrain unaamini kuwa Mashia tu ndio wanaopinga udikteta nchini humo. Ni kwa msingi ndio, kwa kuwapokonya uraia Mashia, utawala wa Aal Khalifa unatekeleza maangamizi ya kimbari au kwa uchache kubadilisha muundo wa kijamii kwa namna ambayo katika siku za usoni, Mashia watabadilika na kuwa jamii ya waliowachache.

Jinai dhidi ya binadamu

Lynn Maalouf Mkuregnezi wa kitengo cha Mashariki ya Kati katika shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International anasema: "Serikali inazidi kuongeza idadi ya watu wanaopokonywa uraia na hivyo kuwaacha wengi bila uraia. Wengi wanalazimishwa kuhama nchi ili kwa njia hiyo kuwakandamiza wapinzani. Utawala wa Bahrain unawalazimisha raia wake kuihama nchi katika hali ambayo, kifungu cha 4 cha Hati ya Kuasisi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kinasema, 'kubaidisha na kulazimisha watu kuhama makao yao ni moja ya misdaki za jinai dhidi ya binadamu."

Utawala wa Aal Khalifa mbali na kuwalazimisha raia wa nchi hiyo kuhama, pia umepitisha au kutekeleza hukumu kadhaa za kuwanyonga wapinzani na waandamanaji. Mwaka 2017, mahakama za utawala wa Bahrain ziliwanyonga raia watatu na hali inazidi kuwa mbaya kwani katika kipindi cha wiki moja iliyopita, mahakama hizo za kidhalimu zimetoa hukumu za kunyongwa raia 22.

Hukumu za kunyongwa kama chombo cha kisiasa

Jumuiya ya Kimataifa ya Haki za Binadamu (FIDH) nayo imetoa taarifa na kutangaza kuwa: "Bahrain inashuhudia ongezeko la kuogofya la hukumu za kunyongwa tokea mwaka 2017 hadi sasa."  Florence Bellivier  Naibu Mkuu wa FIDH anasema hukumu za kunyongwa zinatumiwa kama chombo cha kisiasa na watawala wa Bahrain. Amesema hukumu hizo za kunyongwa zinatolewa kidhalimu na zinatokana na muamala wa kibaguzi na usio wa kibinadamu.
Kutokana na kimya cha madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu na pia Umoja wa Mataifa, hasa chombo chake muhimu zaidi yaani Baraza la Usalama, hivi sasa tunaona ni mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ndiyo yanayoukosoa utawala wa kiimla wa Bahrain kufuatia kushadidi jinai zake dhidi ya wananchi.

3465110

captcha