IQNA

Kiongozi wa Hizbullah atahadharisha kuhusu njama za Marekani

11:32 - February 25, 2018
Habari ID: 3471403
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ametoa wito kwa wananchi wa Lebanon kutowapigia kura wagombea wanaopata himaya ya Marekani katika uchaguzi ujao wa bunge huku akionya kuwa wanasiasa kama hao wasaliti watakaoikabidhi nchi kwa Marekani.

Kiongozi wa Hizbullah atahadharisha kuhusu njama za MarekaniAkihutubia taifa kwa njia ya televisheni akiwa katika mji wa mashariki mwa Lebanon wa Baalbek Jumamosi jioni, Sayyed Hassan Nasrallah ametoa wito kwa watu kutoka amtabaka yote ya taifa kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Mei sita.

Amesema wapiga kura wanapaswa kuzingatia maslahi ya kitaifa wakati wa uchaguzi. Aidha ametoa wito kwa wapiga kura kutochukua maamuzi kwa kuzingatia masuala ya kifamilia, kidini ya chama bali  bali wawachague wale wanaoweza kutumiza majukumu kwa taifa.

Sayyed Nasrallah ameongeza kuwa, watakaogombea ubunge kwa tikezi ya Hizbullah watawaklisha taifa lote la Lebanon si mrengo wao wa kisiasa.

Kiongozi wa Hizbullah amesisitiza kuwa Walebanon hawapaswi kulikabidhi bunge kwa wale watakaotii matakwa ya Marekani au kulegeza msimamo mbele ya utawala haramu wa Israel kuhusu utajiri wa mafuta. Aidha ametahadharisha kuhusu kuwapigia kura watu ambao watapanga njama dhidi ya Hizbullah au wenye nia ya kuvuruga uchumi wa Lebanon. 

Kwingineko katika hotuba yake, Nasrallah ameonya kuhusu njama za Marekani katika eneo la Mashariki ya kati na kusema safari ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani katika eneo imefanyika ili kuendeleza njama hizo chafu.

3465264

captcha