IQNA

Mabingwa Waislamu katika Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza, EPL

21:32 - February 26, 2018
Habari ID: 3471405
TEHRAN (IQNA)- Wiki za hivi karibuni nchini Uingereza, mshambuliaji Muislamu na Mwarabu wa Timu ya Soka ya Liverpool katika Ligi Kuu ya maarufu kama EPL amevuma kwa umahiri na dini yake.

Mabingwa Waislamu katika Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza, EPLMchezaji huyu ni Mohammad Salah ambaye pia ni maarufu kwama 'Mfalme wa Misri' ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora katika Ligi Kuu ya Uingereza hivi sasa na ana wafuasi wengi ambao wanavutiwa na kipaji chake na pia kufungamana kwake na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Mohammad Salah si Mwislamu jina tu, bali ni kijana ambaye hutekeleza mafundisho ya Kiislamu ikiwemo kuswali sala tano kwa siku. Yeye huonekana akiswali akiwa ameandamana na wachezaji wenzake Waislamu ambao ni Sadio Mané na Emre Can na kila anapopachika bao wavuni husujudu kama njia ya kumshukuru Allah SWT kwa kumpa kipaji alichonacho.

Machezaji mwingine maarufu Muislamu na mwenye kipaji katika Ligi Kuu ya Uingereza ni Paul Pogba wa Manchester United ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2016. Man U iliweka rekodi ya kutoa kitita kikubwa zaidi cha fedha kukamilisha usajili wa Pogba kutoka klabu ya Juventus, ambapo ilimsajili kwa dau la Euro milioni 105, na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani. Pogba anafuata mafundisho ya Uislamu kuhusu ukarimu na hutoa sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza katika jamii ya kuchangia miradi mbali mbali ya kijami.

Wachezaji wengine wanaofungamana na mafundisho ya Uislamu Uingereza nia Riyadh Mahrez- ambaye aliisaidia Liecester kushinda Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2016 akiwa na Muislamu mwenzake katika timu hiyo N'Golo Kanté, ambaye sasa anachezea mabingwa watetezi Chelsea. Wachezaji wengine mashuhuri Waislamu katika Ligi Kuu ya Uingereza, EPL, ni Mesut Özil, wa Arsenal, Yaya Touré, Mamadou Sakho wakiwa Crystal Palace, Islam Slimani wa Newcastle… na wengine wengi.

Wachezaji hao Waislamu, kama vile Pogba na Özil wameweka picha katika mitandao ya kijamii wakiwa wameenda kutekeleza Ibada ya Hija mjini Makka na hivyo kuwa mfano mzuri kwa vijana Waislamu ambao ni hodari katika soka na fani nyinginezo.

Pamoja na kuwa Waislamu wametoa mchango mkubwa katika kustawisha viwango cha soka Uingereza lakini kuna kundi lenye chuki dhidi ya Waislamu linalojulikana kama Football Lads Alliance (FLA) ambalo limekuwa likieneza chuki dhidi ya wachezaji Waislamu. Pamoja na hayo, hivi sasa watu wengi wamepevuka na hawasikilizi tena propaganda za makundi hayo bali wanachojali ni kiwango bora cha soka.

3465267

captcha