IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanachuo Saudi Arabia

1:44 - February 28, 2018
Habari ID: 3471409
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Tisa ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Saudi Arabia yamekuwa yakiendelea mjini Jeddah tokea Februari 25.

Mashindano ya Qur'ani ya wanachuo Saudi ArabiaMashindano hayo ya Qur'ani ya siku tano yanajumuisha wanafunzi 500 kutoka vyuo vikuu 21 vya umma katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ya Qur'ani yana kategmoria nne ambao ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20,10 na 5 kwa kuzingatia misingi ya tajwidi.

Waandalizi wametangaza kuwa washindi watatnukiwa zawadi kadhaa zikiwemo fedha taslimu.

Kwa mujibu wa Salahuddin Bauthman, mmoja kati ya wakuu wa kamati andalizi anasema mashindano hayo yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Jeddah ni mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani kwa wanachuo nchini Saudi Arabia.

3694297

captcha