IQNA

0:22 - March 03, 2018
News ID: 3471413
TEHRAN (IQNA)-Waandalizi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Tunisia wameiomba Iran imteue qarii na mtaalamu Qur’ani ili awe miongoni mwa jopo la majaji katika mashindano hayo.

Qarii wa Iran kuwa jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani TunisiaShirika la Wakfu la Iran limethibitisha kupokea mwaliko huo na tayari limemeteua qarii Muirani wa kimataifa kuwa jaaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani nchini Tunisia.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Ali Mughanni amesema mbali na kuteua jaji kuwakilisha Iran katika mashindano hayo ya Tunisia, pia Wairani wawili, Mohammad Javad Muradi na Mohammad Hassan Muwahedi watashiriki katika mashindano hayo kama washindani.

Muradi ataiwakilisha Iran katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani kikamilifu na Muwahedi atashiriki katika kitengo cha qiraa.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tunisia yatafanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis, mwezi Mei.

3695185

Name:
Email:
* Comment: