IQNA

15:03 - March 06, 2018
News ID: 3471419
TEHRAN (IQNA)- Waandishi habari Wapalestina wameandamana nje ya ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Ghaza kulalamikia mwenendo wa mtandao wa kijamii wa Facebook kufunga akaunti za Wapaletina.

Waandishi habari Wapalestina wasema Facebook inashirikiana na IsraelWakiandamana Jumatatu, waandishi habari hao walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa, "Facebook ni mshirika wa jinai za Israel", na "Facebook inapendelea Maghasibu (Israel)".

Akizungumza katika maandamano hayo yaliyoandaliwa na Kamati ya Uungaji Mkono Waandishi Habari Palestina, Salama Maarouf, msemaji wa Hamas, ameitaja Facebook kuwa, "mkiukaji mkubwa wa uhuru wa maoni na kujieleza."

Amesema mwaka 2017, Facebook ilifunga karibu akaunti 200 za Wapalestina na zingine 100 katika mwaka huu wa 2018 chini ya visingizio visivyo na msingi.

Amesema asilimia 20 ya akaunti za Facebook za Waisraeli huchochea wazi wazi vita na chuki dhidi ya Wapalestina pasina kuchukuliwa hatua zozote au kufungwa.

Mwaka 2016, Facebook ilitiliana saini mapatano na utawala haramu wa Israel ambapo iliahidi kudhibiti yaliyomo katika akaunti za Wapalestina.

3465334

Mwezi Machi mwaka 2017, Facebook ilifunga kwa muda akaunti ya Facebook ya chama cha Fatah cha Mamlaka ya Ndnai ya Palestina baada ya kuchapishwa picha ya zamani ya hayati mpigania ukombozi Palestina Yasser Arafat akiwa amebeba bunduki.

Itakumbukwa kuwa mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg ni Yahudi Mmarekani na baba yake ni raia wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

3697331

Name:
Email:
* Comment: