IQNA

12:11 - March 07, 2018
News ID: 3471420
TEHRAN (IQNA)-Hali ya hatari imetangazwa kote Sri Lanka Jumanne baada ya magenge ya Mabuddha kuwahujumu Waislamu katika wilaya moja ya kati mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema machafuko yaliibuka katika wilaya ya Kandy Jumapili baada ya magenge ya Mabuddha kutoka kabila la Sinhal kuushambulia nyumba na biashara za Waislamu na pia msikiti katika eneo hilo. Mtu moja alifariki katika ghasi hizo ambazo zimepelekea serikali kutuma mamia ya wanajeshi eneo la Kandi mbali. Aidha sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika eneo hilo ili kutuliza hali ya mambo.

Hali ya hatari imetangazwa kitaifa baada ya serikali kuhofia kuwa  kuenea ghasia zaidi kufuatia klipu ya sauti iliyorekidowa na kusambazwa kuhusu Mwislamu ambaye aliaga dunia baada ya kukwama katika nyumba iliyokuwa inateketea moto.

Msemaji wa serikali Dayasiri Jayasekera amesema hali ya hatari imetangazwa ili kuzuia ghasia na kuenea katika nchi hiyo ambayo ndio mwanzo inaanza kupata afueni baada ya miongo kadhaa ya vita vya ndani. Amesema hali ya hatari itaendelea kwa muda wa siku 10 huku maafisa wa usalama wakichukua hatua kwa wale wote wanaoenza uchochezi kupitia mitandao.

Mwislamu aliyepoteza maisha baada ya nyumba yake kuteketea moto ametajwa kuwa ni Fayaz Shamsudin. Baba yake amesema waliweza kutoka katika ghorofa ya kwanza wakati moto ulipoanza lakini mwanae aliyekuwa katika ghorofa ya pili hakuweza kunusurika.

Taarifa zinasema wahubiri wa Kibuddha wamekuwa wakichochea hisia za chuki dhidi ya Waislamu na hadi sasa misikiti minne, nyumba 37, maduka 46 na magari 35 ya Waislamu yameteketezwa katika mkoa wa kati.

Sri Lanka ni nchi ya kisiwani katika Asia ya Kusini na iko karibu na ncha ya kusini ya rasi ya Uhindi katika Bahari Hindi.

3465338

Name:
Email:
* Comment: