IQNA

Nakala ya Kale ya Qur’ani yapatikana Tunisia

19:35 - March 19, 2018
Habari ID: 3471435
TEHRAN (IQNA)- Nakala nadra ya na yake ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa karne 9 zilizopita imepatikana nchini Tunisia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, nakala hiyo hivi karibuni ilikabidhiwa Maktaba ya Kitaifa ya Tunisia.

Hii ni moja ya nakala za Qur’ani zinazonasibishwa na mwanakaligrafia mashuhuri wa Andalusia, Ibn Ghatous.

Wataalamu wanaamini kuwa ilichukua miezi sita kwa mwanakaligrafia huyo wa Morocco kuandika nakala hiyo ya Qur’ani.

Mkurugenzi wa nakala za kale katika maktaba hiyo Shakir Adil Kashak amesema jina la mwanakaligrafia huyo limeandikwa kwa dhahabu katika ukurasa wa mwisho wa msahafu huo.

Aidha amesema maktaba hiyo ina nakala zingine mbili za Qur’ani ambazo inaaminika ziliandikwa na Ibn Ghatous.

Kwa mujibu wa Kashak, nakala iliyopatikana hivi karibuni ni ndogo kuliko mbili za awali. Ibn Ghatous aliaga dunia mwaka 1213 Miladia na wanahistoria wanasema aliandika nakala 500 za Qur’ani.

3700948

captcha