IQNA

Utawala dhalimu wa Saudia waendelea kuua watoto, wanawake Yemen

20:38 - March 22, 2018
Habari ID: 3471440
TEHRAN (IQNA)- Ndege za kivita za utawala dhalimu wa Saudia Arabia zimedondosha mabomu katika maeneo ya raia ya mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa Yemen nna kuua na kujeruhiwa raia 17 wakiwemo wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa televisheni ya al-Masirah ya Yemen, ndege hizo za Saudia zilidondosha mabomu katika nyumba za raia wilayani Ghamar mapema leo Alhamisi.

Tukio hilo limejiri siku moja tu baada Jeshi la anga la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah kuitungua ndege ya kivita ya  Saudia katika mji wa Saada.

Baada ya kudondoshwa ndege hiyo ya kivita ya Saudia aina ya F-15 iliyoundwa Marekani, Ibrahim al-Shami, kamanda wa jeshi la anga ya Yemen amesema kuwa, ushindi mbalimbali wa Wayemen dhidi ya mvamizi huyo, utaendelea.

Tangu mwezi Machi mwaka 2015, Saudia, ikisaidiwa na kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa UAE na Marekani ilianzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Yemen kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi.

Raia zaidi ya 14,000 wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia tokea mwezi Aprili mwaka huu.

Halikadhalika kutokana na hujuma hiyo ya Saudia na UAE dhidi ya Yemen, Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 20 kati ya jamii ya watu milioni 25 ya Yemen wanahitajia misaada ya kibinadamu.

/3465433

 

captcha