IQNA

Msikiti mjini Stockholm Sweden wahujumiwa

11:35 - March 23, 2018
Habari ID: 3471441
TEHRAN (IQNA)- Msikiti katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm, umehujumiwa na kuandikwa maandishi na nembo za kibaguzi siku ya Alhamisi.

Taarifa ya wasimamizi wa msikiti inasema nembo kubwa ya Wanazi (swastika) ambayo huashiria ubaguzi iliandikwa katika mlango wa msikiti.

Wasimamizi wa msikiti wamelaani vikali kitendo hicho na kusema msukiti huo umekuwa ukihujumiwa mara kwa mara na magaidi.

"Waumini katika msikiti na jamii kwa ujumle imeshtushwa sana na hujuma hizi. Kwa masikitiko makubwa, pamoja na kuwepo hujuma nyingi sana za kigaidi, serikali haijachukua hatua yoyote ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)," wamesema.

Taarifa zinasema msikiti huo ulishambuliwa na wabaguzi mara 22 mwaka 2017 na tokea mwanzo wa mwaka 2018 kumetekelezwa hujuma 23 msikitini hapo.

Mwezi Septemba mwaka jana msikiti uliteketezwa moto katika mji wa Orebro kusini mwa Sweden katika tukio ambalo lilitekelezwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Msikiti wa Orebro ulijengwa mwaka 2007 katika mtaa wa Vivalla ambao ni makazi ya wahajiri Waislamu kutoka nchi mbali mbali.

Tukio hilo lilikuja baada ya msikiti mwingine kuteketezwa moto katika eneo la Jakobsberg ambalo ni kitongoji cha mji mkuu wa Sweden, Stockholm.

Katika miaka ya hivi karibuni Sweden imeshuhudia ongezeko la watu wenye misimamo ya kibaguz ya Kinazi kiasi cha kufanyika maandamano makubwa ya wanaounga mkono Unazi katika miji mikibuwa kama vile Stockholm na Gothenburg.

3465435

captcha