IQNA

Uturuki yatayarisha tafsiri mpya ya Qur'ani kwa kuhusisha wanasayansi

21:45 - April 03, 2018
1
Habari ID: 3471452
TEHRAN (IQNA)- Idara ya masuala ya kidini nchini Uturuki imetangaza mpango wa kuandika tafsiri mpya ya Qur'ani itakayaondikwa kwa mchango wa wanasayansi.

Hayo yamedokezwa na Profesa Ali Erbas, Mkuu wa Masuala ya Kidini katika Ofisi ya Rais (DIB) ambayo ni maarufu kama Diyanet. Amesema tafsiri hiyo mpya, yenye kutoa maelezo kuhusu maana ya aya za Qur'ani Tukufu, itategemea mchango wa wataalamu katika nyuga mbali mbali za sayansi.

Kwa mfano katika aya zinazohusiana na elimu ya unajimu au falaki (astronomy) wataalamu bingwa wa taaluma hiyo watatoa mchango wao.

Akizungumza Jumatatu mjini Istanbul, Erbas amesema: "Katika Sura Al-Muminun, kuna aya zinazozungumza kuhusu maumbile ya mwanadamu kutoka tone la ya mbegu ya uzazi hadi kuzaliwa mtoto na kwa msingi huo hapo mtaalamu wa masuala  ya ginekologia anaweza kutoa mchango wake ili kuongezwa kiwango cha ufahamu wa aya hizo."

3465478

Habari zinazohusiana
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Sabri Al harthy
0
0
Assalam Aleikum,naomba itapokuwa tayari tafsiri hiyo, nipatiwe katika Email yangu.
captcha