IQNA

Washiriki 24 washindana siku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

14:37 - April 21, 2018
Habari ID: 3471474
TEHRAN (IQNA)- Washiriki 24 katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu wameshindano katika siku ya kwanza ya Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa rasmi Alhamisi 19 Aprili yalianza jana Ijumaa 20 Aprili asubuhi katika Ukumbu wa Sala wa Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran.

Katika mashindano hayo  ya jana ambayo yalikuwa ya mchujo, washiriki saba  waliondolewa baada na waliofuzu wataendelea katika awamu itakayofuata.

Mashindano ya mwaka huu yatajumuisha Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran (ya kawaida maalumu kwa ajili ya wanaume) na pia kutakuwa na mashindano mengine ya Qur'ani ya wanawake, ya wenye ulemavu wa macho, ya wanafunzi wa vyuo vikuu na ya wanachuo wa vyuo vya kidini.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yatafanyika katika miji mitatu ya Tehran, Mashhad na Qum, ni tukio kubwa zaidi linalohusiana na Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu na yamekuwa yakiimarika kila mwaka.

3707276/

captcha