Kwa mujibu wa jopo la majaji, Mohammad Zahedi alishika nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa ya Qur'ani na ufahamu ya misingi ya Qur'ani.
Ali Hassan Abdul Aa’la wa Iraq na Mohammad Reza Nouri wa Afghanistan waliibuka wa pili na wa tatu kwa taratibu.
Katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na ufahamu wa misingi ya Qur'ani, mwakilishi wa Iran Mahamoud Norouzi alishika nafasi ya kwanza. Nafasi ya pili imechukuliwa na Ahmad Yasri wa Misri huku Mohammad Tijani wa Ghana akishika nafasi ya tatu.
Sherehe za kufunga mashindano hayo zilihudhuriwa na wanazuoni wa ngazi za juu wakiwemo mwanazuoni mtajika Ayatullah Jafar Sobhani, mkurugenzi wa vyuo vya kidini vya Kiislamu nchini Iran, Ayatullah Ali Reza Aarafi, and na mkuu wa Shirika la Wakfu, Hujjatul Islam Ali Mohammadi.
Mashindano ya mwaka huu yaliyoafunguliwa rasmi Jumatano iliyopita yanjumuisha Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran (ya kawaida maalumu kwa ajili ya wanaume) na pia kunafanyika mashindano mengine ya Qur'ani ya wanawake, ya wenye ulemavu wa macho, ya wanafunzi wa vyuo vikuu na ya wanachuo wa vyuo vya kidini.
Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani yanayofanyika kwa kaulimbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja" sambamba na kuanza sherehe za mwezi huu mtukufu wa Shaaban yanawajumuisha wasomaji (quraa) na waliohifadhi (hufadh) Qur'ani 258 kutoka nchi 84.
/3708866