IQNA

Iran yahimiza za Kiislamu ziandae mashindano ya Qur'ani ya wanachuo

21:36 - April 28, 2018
Habari ID: 3471486
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo imekuwa mwenyeji wa duru kadhaa za mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu duniani inahimiza nchi zingine za Kiislamu ziandae duru zijazo za mashindano hayo.

Hayo yamedokezwa na Ustadh Rahim Khaki jaji katika Mashidano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanachuo Waislamu wakati akihojiwa na IQNA. Amebaini kuwa Iran imekuwa ikiandaa duru zote za mashidano hayo tokea yaanzishwa ikiwemo ya sita ambayo ilianza Ijumaa katika mji wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran ikitazamiwa kumalizika Jumapili .

Amesema tokea wakati wa duru ya nne ya mashindano hayo, ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili, kumekuwepo na jitihada za kuhimiza nchi zingine ziandae mashindano hayo huku kukiwa na matumaini kuwa  jambo hilo litawezekana katika duru ya saba.

Halikadhalika Ustadh Khaki ameelezea matumaini yake kuwa duru ijayo ya mashindano hayo itajumuisha pia wanafunzi wa kike Waislamu kutoka vyuo vikuu mbali mbali duniani.

Aidha amesema kiwango cha mashindano ya mwaka huu ni bora ikilinganishwa na mashindano yaliyotangulia. Nchi 35 kutoka mabara ya Asia, Afrika, na Ulaya zinawawakilishwa katika mashindano hayo ya wanafunzi Waislamu .

Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3709591

captcha