IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hujuma dhidi ya Yemen ni mfano mwingine wa uhabithi wa mabeberu wa kimataifa

12:45 - June 21, 2018
Habari ID: 3471567
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na nchi kadhaa zenye silaha za kisasa kwa ajili ya kuwanyang'anya watu wanaodhulumiwa wa Yemen bandari ya al Hudaydah kuwa ni mfano mwingine wa uhabithi wa kidhati wa madhalimu na mabeberu wa kimataifa.

Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo mapema Jumatano mjini Tehran katika kikao na spika, wabunge na wafanyakazi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, na kusema: "Maadui hao wa ubinadamu pia wanaifanyia uadui Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sababu ya kusimama kidete na kupigania uadilifu kwa taifa la Iran lakini kwa baraka zake Mwenyezi Mungu, taifa hili litaishinda Marekani na maadui wengine kutokana na kulinda umoja na mshikamano wa ndani."

Kiongozi Muadhamu aliashiria kuendelea kubainika wazi zaidi dhati khabithi ya Marekani na watumiaji mabavu wengine katika uga wa kimataifa na kusema: "Suala hili la kuwatenganisha maelfu ya watoto na wazazi wao nchini Marekani ni kosa kubwa sana. Mtu hawezi kustahamili kusikia vilio vya watoto hao katika televisheni. Lakini pamoja na hayo, kwa ukhabithi mkubwa walionao, Wamarekani wanawatenganisha watoto na wazazi wao wahajiri."

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Bunge la Iran ambalo limebalehe na kukomaa linapaswa kutenda kwa kujitegemea katika kutunga sheria za masuala kama kupambana na ugaidi na mapambano dhidi ya utakatishaji wa fedha chafu. Amesisitiza ulazima wa amesisitiza ulazima wa kukabiliana kiuerevu na baadhi ya mikataba na mapatano ya kimataifa na kuongeza kuwa: "Katika hatua ya kwanza mikataba hiyo hubuniwa na kupikwa katika vikao vya madola makubwa kwa ajili ya kudhamini maslahi yao, kisha hupewa sura ya kimataifa kwa kujiunga nchi waitifaki wa madola hayo, au nchi vibaraka au zile zilizotishwa, kwa kadiri kwamba pale nchi zinazojitawala kama Iran zinapokataa mikataba hiyo hushambuliwa vikali na kwa mfano kuambiwa ni kwa nini zinakataa mkataba uliokubaliwa na nchi 150?

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaini kuwa Marekani na maadui wengine wa taifa la Iran ni watumiaji mabavu kwa maana halisi ya neno hilo na hivyo mfumo wa Kiislamu, taifa na wakuu wa Iran hawatasalimu amri mbele ya utumijaji mabavu huo.

3466127

captcha