IQNA

Marekani inatoa mafunzo kwa magaidi 8,000 ili waibue ghasia Iraq

16:59 - June 26, 2018
1
Habari ID: 3471573
TEHRAN (IQNA)- Mbunge mmoja Muiraqi amefichua kuwa Marekani hivi sasa inatoa mafunzo kwa magaidi 8,000 wa kundi la ISIS nchini Syria ili kuwatumia katika kuibua ghasia mpya nchini Iraq.

Bi. Ferdows Awadi, mwanachama wa Muungano wa Utawala wa Sheria katika Bunge la Iraq, ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za kuzima njama hiyo.

Ametahadharisha kuwa, iwapo serikali haitachukua hatua za dharura, basi baadhi ya maeneo ya Iraq yataanguka mikononi mwa magaidi.

"Hivi sasa kuna njama zinazotekelezwa na Marekani kuhuisha kundi la kigaidi la ISIS ili kuliwezesha kukalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo," amebaini mbunge huyo.

Aidha Awadi amefichua kuwa Wamarekani wanalenga kuitumbukiza Iraq katika vita vipya vya ndani sambamba na kuibua matatizo ya kiuchumi nchini humo.

Ametoa wito kwa Wairaqi kukabiliana na njama hiyo, ambayo pia inalenga wapiganaji wa kundi la kujitolea la wananchi, Al Hashd al Shaabi.

Mwezi Disemba mwaka 2017, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al Abadi alitangaza kumalizika oparesheni ya miaka mitatu ya wanajeshi wa nchi hiyo kuwatimua magaidi wa ISIS. Oparesheni hiyo ilifanikiwa kwa msaada wa wapiganaji wa Al Hashd al Shaabi.

3466162

Kishikizo: iqna
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Sabri Al Harthy
0
0
Nafatilia sana habari zenu kwani ni zauhakika, naomba kupata au munitumie web ambayo nitapata matangazo yenu ya Radio Iran niyapate moja kwa moja, mimi nipo Ujerumani. Ahsanteni sana
captcha