IQNA

Al-Sudais akosolewa msikitni Geneva kutokana na mauaji ya Saudia Yemen

22:57 - July 04, 2018
Habari ID: 3471583
TEHRAN (IQNA)- Video imesambaa katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha Imamu wa Msikiti wa Makka nchini Saudia, Sheikh Abdul Raham al-Sudais akikosolewa vikali nchini Uswisi kutokana na sera za Saudia za kuihujumu Yemen na kuiwekea Qatar mzingiro.

Kwa mujibu wa taarifa, al-Sudais ambaye ni mfanyakazi wa utawala wa Saudia, aliulizwa maswali magumu na mmoja wa waumini waliofika kusikiliza hotuba yake katika msikiti mmoja mjini Geneva lakini hakuwa tayari kujibu maswali hayo. Mwislamu aliyekuwa na hasira anasikika  katika video hiyo akimuuliza  al-Sudais hivi: “Ni vipi unahubiri kuhusu amani wakati munawawekea mzingiro na kuwanyima chakula ndugu zenu Yemen na Qatar?”

Al Sudais anaonekana akitoka katika msikiti pasina kujibu maswali ya mwenye kuuliza. Mwislamu huyo aliyepata ujasiri wa kumuuliza al-Sudais ni raia wa Algeria na alimtaka pia ajibu kuhusu kuhusika Saudia katika mapindizu ya serikali za Algeria mwaka 1992 na pia mapinduzi ya miaka ya hivi karibuni huko Misri na Uturuki.  Aidha  Mualgeria huyo aliituhumu Saudia kuwa inashirikiana na Marekani katika kuvuruga  amani huku akimtaja al-Sudais kuwa mhubiri wa urongo ambaye anatoa fatua za kuhalalisha mauaji ya Waislamu nchini Yemen. Wakati baadhi ya hadhirina msikitini walipojaribu kumyanamzisha wakidai kuwa kauli yake inaibua fitinah, alijibu kwa kusema kunyamaza kimya ni fitina huku akiitaja Saudia kuwa mtumwa wa Marekani.

/3466208

captcha