IQNA

Wagombea ubunge Ache Indonesia sharti kufanya mtihani wa usomaji Qur'ani

21:26 - July 17, 2018
Habari ID: 3471597
TEHRAN (IQNA) – Wagombea ubunge katika mji la Lhokseumawe katika jimbo la Acheh nchini Indonesia wameshiriki katika mtihani wa kusoma Qur'ani Tukufu kama sharti la kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.

Wagombea ubunge Ache Indonesia sharti kufanya mtihani wa usomaji Qur'ani

TEHRAN (IQNA) – Wagombea ubunge katika mji la Lhokseumawe katika jimbo la Acheh nchini Indonesia wameshiriki katika mtihani wa kusoma Qur'ani Tukufu kama sharti la kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.

Tume Huru ya Uchaguzi ya Lhokseumawe imesema wagombea wa vyama sita ambavyo ni Chama cha Kitaifa cha Mwamko (PKB), Chama cha Garuda, Chama cha Mapambano ya Kidemokarsia (PDI-P), Chama cha Golkar na Chama cha Nasdem, wamefanyiwa mtihani siku ya Jumatatu. Mitihani ya vyama vyote ilipangwa kumalizika Julai 18. Watahiniwa wanaulizwa maswali kuhusu adab, tajwid na ufasaha wa kusoma Qur'ani Tukufu na mitihani hiyo imesimamiwa na Idara ya Qiraa ya Qur'ani katika mji wa Lhokseumawe, Baraza la Maulamaa na Wizara ya Masuala ya Kidini.

Kwa mujibu wa sharia ya 1999 ya hali maalumu ya eneo la Aceh, pamoja na Sheria yam waka 2001 ya Mamlaka Maalumu ya Kujitawala Aceh, eneo hilo ndio pekee ambalo linaruhusiwa kutekeleza kikamilifu sharia za Kiislamu nchini Indonesia.

Kwa mujibu wa kanuni zilizopo, wagombea  wote  wa vitu vya ubunge na serikali za mitaa wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma Qur'ani Tukufu.

Indonesia ni nchi ya visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Uhindi na Pasifiki. Visiwa vyake ni sehemu ya funguvisiwa ya Malay. Aidha Indonesia ni nchi ya visiwa 18,000 ilhali zaidi ya 6,000 kati ya hivyo vinakaliwa na watu.Indonesia pia inatajwa kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani. Kati ya watu milioni 261 nchini Indonesia karibu milioni 225 ni Waislamu.

3466292/

captcha