IQNA

Waislamu Uswizi walalamikia ubaguzi

11:07 - July 19, 2018
Habari ID: 3471600
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Uswizi wamelalamikia ubaguzi unaotokana na kuunasibisha Uislamu na utumiaji mabavu.

Katika taarifa, Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Uswizi umeonya kuhusu kunasibisha utumiaji mabavu na dini tukufu ya Kiislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.

Katika mahojiano na gazeti la Neue Zürcher Zeitung siku ya Jumanne, msemaji wa muungnaohuo Pascal Gemperli amesema dini ya mtu haipaswi kutumiwa kubaini iwapo yeye ni mhalifu au la. Amesema mabarobaro Waislamu wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa katika mahakama za watoto pasina kuwa na mawakili katika hali ambayo mabarobaro wa dini zinginezo wanapata haki zaidi katika mahakama hizo.

Aidha amesema Uislamu ni dini kubwa lakini sasa inatizwam kwa jico tu la ugaidi na misimamo mikali. Aidha amesema tokea mwaka 2013 kumshuhudiwa ongezeko maradufu la vitendo vya kubaguliwa Waislamu.

Gemperli amesema baada ya matukio ya Septemba 11 mwaka 2001, Waislamu Uswizi wamekuwa wakitazamwa kama chanzo cha tatuzi huku hata baadhi wakisema Mswizi halisi hawezi kuwa Mwislamu. Amesema umma unapaswa kufahamishwa kuwa Uislamu ni mojawapo kati ya dini za Uswizi.

3466295

captcha