IQNA

Maonyesho ya 30 ya Kitaifa ya Sanaa za Mkono Iran yalifunguliwa Jumamosi 25 Agosti 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Maonyesho mjini Tehran. Katika maonyesho hayo kumezinduliwa athari za Sirr al-Asrar ambazo msingi wake ni riyawa kuhusu fadhila za Amirul Muminin Ali AS ambazo zimeandikwa kwa maandishi ya Thulath, Nastalikh na Kufi kwa mbinu za Kiirani za Kalamkari na Negargari.