IQNA

10:49 - September 06, 2018
News ID: 3471661
TEHRAN (IQNA)- Kongamano lenye anuani ya "Mtume wa Rahma' limefanyika nchini Uganda kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Iran, Shirika la Utangazaji lwa Uganda (UBC) na Baraza Kuu la Waislamu Uganda (UMSC).

Kongamano hilo limefanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Uganda General Moses Ali, Balozi wa Iran nchini Uganda Mortadha Murtadhawi, Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda Ali Bakhtiari, Naibu Muftu wa Ugada Profesa Kateregga, wahadhiri wa vyuo vikuu pamoja na wanafunzi Waislamu na Wakristo kutoka vyuo vikuu.

Akihutubu katika kikao hicho, balozi wa Iran amesema makongamano kama hayo ni muhimu katika kaungazia Sira na maisha ya Mtume Muhammad SAW.

Naye Naibu Mufti wa Uganda ameashiria kutajwa Mtume Muhammad SAW katika Qur'ani Tukufu kama 'Mtume wa Rahma" na kutoa wito kwa watu wote kufuata mafundisho ya Mtume SAW ili kuleta umoja na kusitisha uhasama duniani.

Naye Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bakhtiari ameashiria aya za Qur'ani Tukufu zinazomtaja Mtume SAW kuwa ni Rahma si tu kwa Waislamu bali kwa dunia nzima.

Naibu Waziri Mkuu wa Uganda Jenerali Moses Ali pia alihutubu katika sherehe za kufunga kongamano hilo ambapo alisisitiza kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

3743947

Name:
Email:
* Comment: