IQNA

Msikiti wa Wazir Khan uko katika mji wa Lahore, makao makuu ya mkoa wa Punjab nchini Pakistan na ujenzi wake ulianza mwaka 1634 na kumalizika 1641 Miladia wakati wa utawala wa Shah Jahan. Msikiti huo umetajwa kuwa miongoni mwa misikiti iliyopwamba vizuri zaidi katika zama hizo za silsila ya Mughal au Gurkani.