IQNA

Waislamu wa Madhehebu ya Sunni Iran washiriki ziara katika Haram ya Imam Ridha AS

9:55 - November 07, 2018
Habari ID: 3471732
TEHRAN (IQNA)- Maulamaa na Waislamu wa matabaka mbali mbali wa madhehebu ya Sunni nchini Iran wameungana na wenzao wa Kishia kufanya ziara katika Haram ya Imam Ridha AS , mmoja wa wajukuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW ambaye pia ni Imam wa Nane wa Waislamu wa Kishia.

Waislamu wote wanampenda Bwana Mtume SAW na Ahlul Bayt wake watoharifu, ni hii ni nguzo muhimu ya kukurubisha Waislamu wa madhehebu zote.
Wakiwa na nyuso za bashasha na furaha, Waislamu hao wa Kisuni wa Iran hufanya ziara hiyo kila mwaka, katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran, ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad SAW wanawahusu Waislamu wote bali kila mpenda haki duniani.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Katika siku ya mwisho ya mwezi wa Safar miaka 1237 iliyopita, aliuawa shahidi Imam Ali bin Mussa Ridha AS, mmoja kati ya wajukuu wa Mtume Mtukufu SAW. Mtukufu huyo alizaliwa mwaka 148 Hijria katika mji wa Madina na kuchukua jukumu la kuongoza Umma wa Kiislamu baada ya kuuawa shahidi baba yake, yaani Imam Mussa al Kadhim AS. Mnamo mwaka 200 Hijria, Maamun, Khalifa wa Bani Abbasi, alimtaka Imam Ridha AS aelekee kwenye makao yake yaliyokuwa katika mji wa Marwi, kusini mashariki mwa Turkemenistan ambayo ilikuwa sehemu ya Khorasan Kuu. Ijapokuwa kidhahiri Maamun alimfanya Imam Ridha kuwa mrithi wake, lakini kwa njia hiyo alikusudia kuimarisha zaidi nguvu za utawala wake. Utukufu na daraja ya juu ya kielimu na kimaanawi aliyokuwa nayo Imam Ridha na ushawishi wake uliokuwa ukiongezeka siku hadi siku ndani ya fikra na nyoyo za watu, vilimtia woga na hofu Maamun, na hivyo akaamua kufanya njama za kumpa sumu na kumuua shahidi Imam Ridha AS. Tunaashiria nasaha ya Imam Ridha AS aliposema:"Mja bora zaidi ni yule ambaye kila anapofanya jema hufurahia, na kila anapokosea huomba msamaha, inapomfikia neema hushukuru, anapokumbana na masaibu husubiri na wakati anapoghadhibika husamehe."

3467161

captcha